JINSI YA KU-FLASH SIMU ZA TECNO

Kabla ya kuanza kujifunza jinsi ya kuflash simu za Tecno za Android ni vyema kujifunza maana ya baadhi ya maneno ili uweze kuelewa kinachofanyika hapa. Kwa kuanza twende tukaangalie nii maana ya neon Flash au fundi anaposema ana flash simu ana maana gani.
Kuflash simu ni nini ?
Kuflash simu ni neno  linalo tumiwa na mafundi simu likiwa na maana ya tendo la kurudisha au ku-repair mfomo au sehemu ya mfumo wa uendeshaji kwa kuinstall Copy ya mfumo huo ili kufanya simu yako kufanya kazi kama inayotakiwa.

MAHITAJI MUHIMU

1.    USB Data Cable
2.    MT6577 USB VCOM Drivers (Win7/8 na Vista)
3.    SP FLASH TOOl – DOWNLOAD HAPA
4.    ROM ZA TECNO – DOWNLOAD HAPA
5.    Computer – Laptop au Desktop

HATUA

1.    Zima simu yako na utoe betri ya simu yako kama simu yako batrery yake ni ya ndani hakikisha umezima kabisa simu yako.
2.    Fungua program ya SP flash tool

http://i1081.photobucket.com/albums/j360/connected/

3.    Kasha baada ya program hiyo kufunguka bofya palipo andiwa SCATTER LOADING iliyopo upande wa kulia chini kidogo.
4.    Baada ya hapo chagua mahali palipo hifadhiwa ROM ya simu yako. Kumbuka kuwa mara nyingi  file hili linakuwa na format ya txt mfano “MTK6577_Android_Scatter_emmc.txt kumbuka chagua file linalo endana na simu yako.
5.    Weka tiki kwenye vyumba vyote isipo kuwa chumba kilicha andikwa Preloader na DSP_bl hapa ni vyema kwuwa makini ili usiharibu simu yako
6.    Baada ya hapo toa betri kwenye simu yako kasha bonyeza YES kwenye program ya SP FLASH Tool
7.    Kasha haraka chomeka simu yako kasha bofya vibonyezo hivi pamoja vibonyezo ( button) zote mbili za sauti pamoja na cha kuwasha yaani power button.
Baada ya kufuata hatua zote hizo kwa makini utaona simu yako ikianza kupokea File kutoka kwenye Computer. Subiri mpaka imalize na  kama ulifuata hatua sawa utaona meseji ikisema “You have successfully restored the Stock ROM”.

Hapo utakuwa umekwisha flash simu yako