Simu zetu za Android zimekua sehemu
ya Maisha yetu ya kila siku. Tunazitumia katika Mawasiliano, Kuhifadhi
kumbukumbu za muhimu, burudani, biashara, nk. Haya yote hufanywa na Program
ambazo huwekwa kwenye mfumo wa simu (Operating System). Programu hizo hubeba
maaginzo maalum (Set of instructions) ambazo humwezesha mtumiaji kufanyia mambo
mbalimbali kutegemea program hio. Mfano wa program muhimu kwenye simu ni kama
vile Opera Mini (humwezesha mtumiaji kufungua kurasa mbalimbali za Intaneti),
Calculator, nk.
Program hizo huwekwa sio tu kwenye
simu, bali hata vifaa vingine kama vile Computer. Mtumiaji wa Simu au Computer
ndie anaeamua program ya kuweka kutegemeana na matumizi yake. Katika miongo
michache iliopita zimetengenezwa program nyingi mpya na zenye maboresho makubwa
na ya kisasa. Ubunifu uliopo katika program mbalimbali unaleta ukuaji katika
Nyanja mbalimbali katika maisha yetu ya kila siku. Program hizi pia zimeleta
urahisi na ufanisi. Mfano Calculator, Saa, Vitabu Vitakatifu (Biblia na Kuran),
Kamusi, Camera, nk.. vyote vimetengenezewa PROGRAM na kuwa rahisi
kuvitumia katika simu muda wowote, mahali popote.
ANDROID NI
NINI..??
Android ni Mfumo wa simu (Operating System) ambao unaboreshwa siku hadi
siku. Mfumo huu una majina tofauti kutegeana na toleo lake. Haya ni Matoleo
(Versions) mbalimbali ya Android kuanzia ya kwanza mpaka ya mwisho;
1. Cupcake
(1.5)
2. Donut
(1.6)
3. Éclair
(2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2
– 2.2.3)
5. Gingerread
(2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb
(3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream
Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean
(4.1 – 4.3.1)
9. KitKat
(4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop
(5.0 – 5.1.1)
Matoleo haya huboreshwa kadri
yanavyozidi kutolewa. Kujua toleo la simu yako nenda Settings – About phone –
Android Version. Ukikuta Jelly Bean, KitKat au Lollipop hongeara! kwani unatumia matoleo ya mwisho yalioboreshwa!!
Mfumo huu wa Android unafaa
kufanyiwa settings mbalimbali na kuwekewa Program mbalimbali ili kumfanya
mtumiaji aifurahie simu yake kwa asilimia 100, lakini shida huja kwamba sio
kila PROGRAM inayowekwa katika mfumo huu wa Android inakubali kufanya kazi!!
Wapo watengenezaji wengi wa program (Software Designers) ulimwenguni. Sasa
watengenezaji wa mfumo huu wa Android wamezuia Program ambazo hazijatoka kwao
zisifanye kazi kwenye mfumo huo kwa sababu za kimaslahi.
HAPA SASA
TUTAPATA KUELEWA MAANA YA KU ‘ROOT’
kua ni
kuifanya simu ikubali Program zilizozuiwa na watengenezaji wa Android (Android
Developers). Ukishai ‘root’ simu yako sasa utakua na uwezo wa kuweka program
zinazohitaji ‘root permission’ kwenye simu yako.
JINSI YA KU
‘ROOT’ SIMU YAKO.
Kuna aina za simu ni rahisi sana ku
root, lakini nyingine zinahitaji utafiti wa kina na muda wa kutosha. Zipo
program nyingi sana zinazoweza kutusaidia zoezi hili. Mojawapo ya Program
ambazo zinajulikana sana kwa ku root simu ni kama vile KingRoot, Vroot, Kingoapp Root,
SRSRoot, Framaroot, Root Master, z4root, Universal root, Easy root, nk.. Baadhi ya Program hizi zitahitaji Computer, nyingine
hazihitaji.
Katika Makala hii tutaelekeza kwa
kutumia Program iitwayi KingRoot ambayo inakubali kufanikisha zoezi hili kwenye
asilimia kubwa ya simu za Android. Program hii haihitaji Computer. Kuipata
nenda Google kisha I isearch na kui download. Kwa msaada uliza……
Maandalizi:
(i) Charge Simu yako, angalao ijae
kwa 50%
(ii) Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako. Menu hii imefichwa kwa watumiaji wa kawaida.
Sisi tunataka kutumia simu zetu kwa 100%. Sasa kuifichua nenda Settings>About
phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na
HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo mara saba (tap 7
times)…mpaka uambiwe “You
are now a Developer”
(iii) Sasa nenda Settings>Developer
options>USB debugging. Weka tiki hapo (kama
haipo)
(iv) Nenda settings>Security>Unknown
Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
Hapo maandalizi yatakua ni tayari.
Sasa download KingRoot 4.0
(or above) kwa kui search kwenye Google kisha Install kwenye simu yako. Baada ya ku install gusa ‘Open’. Baada ya hapo KingRoot itafunguka na itaitambua
simu yako automatically—Model ya Simu na Toleo lake. (Mf. Model: H6 Android
4.4.2). Kama simu yako haijawahi kuwa rooted utaona ‘Root access is
unavailable’. Chini gusa ‘START
ROOT’. Hapo KingRoot itakua
inakomboa simu yako kutoka kwenye kifungo cha maisha…kuwa na subira zoezi hilo
litachukua muda kidogo (sio Zaidi ya dak 6)…mpaka utakapoona ‘ROOT
SUCCSSFULLT’ DONE!!!!! YOU ARE NOW A SUPERUSER…!!!!!
Ili kuhakikisha kama simu yako
imeshakuwa rooted, nenda PlayStore kisha download Root Checker. Ukishai Install na kuifungua gusa ‘VERIFY ROOT’. Ukiona ‘’Congratulations! Root access is properly installed on this
Device” HAPO KILA KITU TAYARI!!!!!
FAIDA ZA KU
ROOT SIMU:
1. Utaweza ku update toleo la mfumo
wa simu yako (Kuflash). Mfano kama unatomia Android 4.4.2 (KitKat) unaweza kui
update kwenda Android 5.0 (Lollipop) Simu ya Android haiwezi kuflashiwa bila
kuwa rooted!
2. Hua inatokea simu kuibiwa. Wewe
unaesoma Makala hii usiibe simu ya Android siku hizi (ukiokota mtafute mwenye
nayo). Nitafute nikupe story!! Sasa zipo program nyingi za ku track simu yako
wakati imeibiwa lakini nyingi huondoka kwenye System ya simu yako baada ya
kufanyiwa ‘Factory reset’ au kuflashiwa. Kama ume root simu yako, zipo Program
za kuitafuta simu yako ambazo hata mtuhumiwa aiflash au aireset….BADO ITAKUWEPO TU! Mfano wa Program hizo ni
Cerberus.
3. Utakua na uwezo wa kuweka Program
nyingi na nzuri za kuifanya simu yako iwe fasta na kuboresha muonekano
(performance and appearance). Pia kuna program za kutunzia chaji, Kuzuia
matangazo kutoka Google (mf. AdAway), n.k…. ambazo hazitafanya kazi bila root
MUHIMU;
Rooting inaweza kuharibu kabisa simu yako na
kuifanya isiwake tena!! (Mimi hapa sitahusika kwa lolote). Usiogope, hii
huwatokea wale wanaokurupuka na kutofuata maelekezo. Mimi binafsi nishairoot
simu yangu na za Marafiki zangu zisizopungua 20 bila madhara yoyote kutokea.
Fanya utafiti kwanza ni program gani sahihi ku root simu yako, omba ushauri,…..
Pia Rooting inaharibu Warranty ya
simu yako. Kama ulipewa Warranty uliponunua simu yako na ukaikuta na tatizo,
ukiirudisha haitakubalika. Aidha, inawezekana pia ku’unroot’
MWISHO;
Kwa yeyote ambae ni mdadisi na mtafiti, anaependa kusaidiwa na Technologia, kuna ulazima wa kuroot simu yake. Baada ya Makala hii, wale woote ambao tutaenda sambamba tutaanza kupitia Programs nyingi ambazo zinahitaji ‘Root Permission’. Mie natumia Tecno M3 , baada ya kui root nimeifanyia Settings nyingi sana na ninaitumia katika mambo mengi sana!! ROOTING imeniwezesha hata kubadilisha muonekano wa maandishi system nzimagg