Kabla ya
kuanza kujifunza jinsi ya kuflash simu za Tecno za Android ni vyema kujifunza
maana ya baadhi ya maneno ili uweze kuelewa kinachofanyika hapa. Kwa kuanza
twende tukaangalie nii maana ya neon Flash au fundi anaposema ana flash simu
ana maana gani.
Kuflash simu
ni nini ?
Kuflash simu
ni neno linalo tumiwa na mafundi simu
likiwa na maana ya tendo la kurudisha au ku-repair mfomo au sehemu ya mfumo wa
uendeshaji kwa kuinstall Copy ya mfumo huo ili kufanya simu yako kufanya kazi
kama inayotakiwa.
MAHITAJI
MUHIMU
1. USB Data Cable
2. MT6577 USB VCOM Drivers (Win7/8 na
Vista)
3. SP FLASH TOOl – DOWNLOAD HAPA
4. ROM ZA TECNO – DOWNLOAD HAPA
5. Computer – Laptop au Desktop
HATUA
1. Zima simu yako na utoe betri ya simu
yako kama simu yako batrery yake ni ya ndani hakikisha umezima kabisa simu
yako.
2. Fungua program ya SP flash tool
3. Kasha baada ya program hiyo kufunguka
bofya palipo andiwa SCATTER LOADING iliyopo upande wa kulia chini kidogo.
4. Baada ya hapo chagua mahali palipo
hifadhiwa ROM ya simu yako. Kumbuka kuwa mara nyingi file hili linakuwa na format ya txt mfano “MTK6577_Android_Scatter_emmc.txt
kumbuka chagua file linalo endana na simu yako.
5. Weka tiki kwenye vyumba vyote isipo
kuwa chumba kilicha andikwa Preloader na DSP_bl hapa ni vyema kwuwa makini ili
usiharibu simu yako
6. Baada ya hapo toa betri kwenye simu
yako kasha bonyeza YES kwenye program ya SP FLASH Tool
7. Kasha haraka chomeka simu yako kasha bofya
vibonyezo hivi pamoja vibonyezo ( button) zote mbili za sauti pamoja na cha
kuwasha yaani power button.
Baada ya kufuata hatua zote hizo kwa makini utaona simu yako
ikianza kupokea File kutoka kwenye Computer. Subiri mpaka imalize na kama ulifuata hatua sawa utaona meseji
ikisema “You have successfully restored the Stock ROM”.
Hapo utakuwa umekwisha flash simu yako